KOCHA wa Simba Sven Vandenbroeck amewasisitiza wachezaji wake kucheza kwa umoja ili kuendelea kupata ushindi utakaorudisha furaha kwa mashabiki na kutimiza malengo ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza Dar es Salaam amesema pamoja na kwamba wamekuwa wakiongoza ligi hiyo kwa utofauti pointi sita dhidi ya Azam na kushinda michezo yao iliyopita, lakini bado ajafurahishwa na ushindi huo pamoja na kiwango kinachooneshwa na wachezaji wake.
“Nahitaji wachezaji wangu wacheze kwa umoja ili kuendelea kupata ushindi utakao kuwa unarudisha furaha kwa mashabiki na kutimiza malengo yetu ya kutetea ubingwa wa ligi,” alisema Sven.
Amesema bado anatafuta mbinu ya kuinua ari ya wachezaji ili waweze kuendelea kufanya vizuri uwanjani ili kupeleka furaha kwa wapenzi na mashabiki
wa timu hiyo.
Sven amesema bado anatamani timu yake ifunge mabao mengi na kutoruhusu wapinzani wao kufunga bao lolote, ambapo anaamini kuwa kama kutakuwa na umoja, hilo linawezekana.
Kocha huyo ametolea mfano mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC walioshinda wa kitokea nyuma kwa mabao 2-1 wachezaji wake kunawakati walionekana wanategea kupokonya mipira hali iliyosabibisha lango lao wakati mwingi kuwa katika hatari.
“Changamoto hii nitaifanyia kazi kwenye mazoezi ikiwa ni maandalizi yetu kuelekea kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union ya Tanga kuhakikisha tunatumia kila nafasi kupata bao,” amesema Sven.
Post a Comment