KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa kukosekana kwa Kelvin Yondani kwenye mechi zake tatu ambazo ni sawa dakika 270 ni kutokana na tatizo kusumbuliwa na maumivu ya tumbo, atarejea uwanjani akipona.
Yondani alikosekana kwenye kwenye mechi dhidi ya Azam FC , Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na ule dhidi ya Singida United, Uwanja wa Namfua Yanga ilishinda mabao 3-1 kabla ya Juzi, Januari 26 kushinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons.
"Hakuwa sehemu ya timu iliyocheza na Singida Uited kwa kuwa hakusafiri na timu, pia aliniambia kwamba anaumwa hivyo hawezi kucheza kwa sasa," amesema.
Mabao kwenye mchezo wa Juzi, Uwanja wa Taifa yalifungwa na mshambuliaji mpya wa Yanga, Bernard Morrison, raia wa Ghana dakika ya 10 na Ykipe Gnamien raia wa Ivory Coast dakika ya 63 akimalizia pasi ya Morrison ambaye amekuwa gumzo kutokana na uwezo wake wa kuchezea mpira uwanjani.
Post a Comment