RAMADHAN Kabwili, mlinda mlango namba tatu wa Yanga amesema kuwa kuna viongozi ambao amedai kuwa walikuwa ni wa Simba walimfuata na kutaka kumpa gari aina ya Toyota IST.
Kabwili ameyasema hayo kwenye moja ya kituo cha radio alipokuwa akizungumza kwa kueleza kuwa lengo kubwa lilikuwa ni kufanya makusudi ili apate kadi ya njano ya tatu ili asicheze kwenye mechi dhidi ya Simba.
Amesema kuwa Simba walikuwa wanataka akae kipa raia wa Congo, Klaus Kindoki.
"Wakati huo nilikuwa na kadi mbili za njano, lakini sikufanya hivyo kwa kuwa haya si mambo yangu," alisema Kabwili akihojiwa na EA Radio.
Kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa msimu uliopita Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda bao 1-0 lililopachikwa na Meddie Kagere
Post a Comment