Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison amesema anapofanya mbwembwe uwanjani halengi kuwadhihaki timu pinzani bali ni mahsusi kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki ambao wamelipa viingilio kuingia uwanjani

Aidha Bernard ameongeza kuwa hatafanya matukio hayo wakati wote, isipokuwa pale ambapo timu iko kwenye mazingira ya uhakika wa kuondoka na ushindi. Morrison ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kocha Luc Eymael kueleza kutofurahishwa na matukio hayo ambayo aliyafananisha na dhihaka kwa timu pinzani

"Mashabiki wanakuja uwanjani kuona timu yao inashinda, ndio maana wanalipa viingilio, lakini ninapoona timu inaongoza vizuri huwa naona ni bora kufanya kitu ambacho kitawapa burudani zaidi mashabiki wakienda nyumbani wapate cha kusimulia zaidi,"

"Nafikiri kocha yeyote hawezi kukubali hilo moja kwa moja, namheshimu kocha wangu (Eymael) kwa alichoniambia, lakini kwangu nafikiri kuna kitu cha ziada natakiwa kukifanya kama mchezaji, sidhani kama naweza kuacha lakini nitakuwa makini wakati gani nafanya hivyo"
Amesema Morrison.

Imeandaliwa na Yossima Sitta

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.