SVEN Vandenboeck, Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgiji ana mechi tatu za ligi sawa na dakika 270 za moto ndani ya Simba kuweka rekodi yake mpya kutokana na ugumu wa mechi zake zilizobaki.
Simba ikiwa nafasi ya kwanza kwenye ligi na pointi zake 41 imecheza mechi 16 imebakiza mechi tatu kukamilisha mzunguko wa kwanza ambazo zote ni za moto kwa Sven kuweka rekodi yake mpya ndani ya mechi zake tisa za awali.
Endapo atashinda mechi zake zote tatu zilizobaki ama kulazimisha sare ndani ya mechi hizo atapindua meza kibabe na kuipoteza rekodi ya mtangulizi wake Patrick Aussems ambaye kwenye mechi zake tisa za mwanzo alipoteza mechi yake ya nne mbele ya Mbao FC kwa kufungwa bao 1-0.
Mechi zake tatu zilizobaki ni dhidi ya Coastal Union ya Tanga iliyo chini ya Juma Mgunda, Namungo ya Lindi iliyo chini ya Thiery Hitimana na Polisi Tanzania ya Moshi iliyo chini ya Malale Hamsini
Post a Comment