MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Azam FC leo wamepenya hatua ya 32 bora na kuibukia hatua ya 16 bora kwenye michuano ya kombe hilo kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Friend Rangers.
Mchezo huo ulichezwa leo, Januari,27, Uwanja wa Uhuru ulikuwa ni wa ushindani kwa timu zote mbili.
Azam FC walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga Lipuli FC bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali na bao pekee la ushindi lilifungwa na Obrey Chirwa.
Kwa ushindi huo Azam FC inatinga hatua ya 16 bora na itamenyana na Ihefu ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza
Post a Comment