STAA wa Juventus, Cristiano Ronaldo, amesema kitendo cha wao kushinda dhidi ya Parma kimezidi kuongeza gepu na wapinzani wao Inter Milan.
Juventus inaongoza Serie A ikiwa na pointi 51, ikiiacha Inter Milan pointi nne ambayo inashika nafasi ya pili. Inter ina pointi 47 na zote zimecheza mechi 20.
Katika mchezo huo uliochezwa wikiendi iliyopita, Juventus iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku Ronaldo akifunga mabao yote upande wa Juventus.
“Ilikuwa ni muhimu sisi kupata ushindi mbele ya Parma kwa sababu Inter tayari walikuwa wametoka sare na Lazio, ilibidi kushinda ili kuwaacha mbali wapinzani wetu.
“Parma ni timu nzuri ambayo imejipanga na sio rahisi kufungika, lakini tulipambana kwa uwezo wetu tukafanikiwa mbele yao,” alisema Ronaldo.
Ronaldo kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa ufungaji katika Serie A baada ya kufunga mabao 16 akiwa nyuma ya kinara Ciro Immobile wa Lazio mwenye 23.
Post a Comment