LICHA ya kuwa mzuri katika kusaidia kupika mabao, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amempa majukumu mapya winga wake Mghana, Bernard Morrison kuhakikisha kuwa anahusika katika ufungaji kutokana na kikosi hicho kutokuwa na umaliziaji mzuri.
Morrison alionyesha uwezo mkubwa kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi aliyocheza Jumatano hii dhidi ya Singida United ambapo kwenye mechi hiyo alihusika katika mabao mawili ikiwemo krosi moja aliyofunga Haruna Niyonzima.
“Tumekuwa na upotevu wa nafasi ambazo tunazitengeneza, kwa sababu kama utaangalia tunapata zaidi ya nafasi tano lakini hatuzitumii vile ambavyo inatakiwa.
“Kwa hiyo ni wazi sasa wachezaji wangu wanatakiwa kubadilika na kuwa makini katika umaliziaji wa jambo hilo. Kwa Morrison alionyesha uwezo wa kutoa pasi lakini kwa sasa naye anatakiwa kuhusika kwenye kufunga kwa sababu ana uwezo a kufanya hivyo.
Post a Comment