ACHANA na idadi ya mabao ambayo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara waliyapata  mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa, unaambiwa Simba walikuwa wanawaringishia watani wao Yanga kwamba wamewazidi pointi 16.
Ushindi walioupata kwa mpira wa pasi za uhakika kwa wachezaji wote wa Simba wa mabao 3-2 mbele ya Namungo umetosha kuwafanya wazidi kutamba kwamba wao wanaweza kuwa mbali zaidi ya Yanga kwa kuwa wamejijengea ufalme wa pointi 16 ambazo Yanga wanatakiwa kuzishusha ili kuwashusha.
Udambwiudambwi wa Sharaf Shiboub ulikuwa kivutio kwa mashabiki ambao walianza kumshangaa Ibrahim Ajibu ambaye ameanza kunoga taratibu kuunda mfumo wake ndani ya Simba baada ya kumpa pasi Shomari Kapombe aliyemwanga majaro yaliyokutana na bichwa la Francis Kahata aliyelisindikiza jumla nyavuni hiyo ilikuwa dakika ya 21.
Namungo walitumia dakika 14 kusawazisha bao hilo baada ya safu ya mabeki ya Simba kujichanganya  wote wakiwa ndani ya 18 wakabaki wakiusindikiza kwa macho mpira wa krosi iliyopigwa na Relliants Lusajo ikazamishwa kimiani na Bigirimana Blaise aliyemtungua Beno Kakolanya.
Hassan Dilunga aliwanyanyua mashabiki wa Simba dakika tatu mbele akimalizia pasi ya Meddie Kagere kwa kufunga bao la pili  akiwa nje ya 18 kwa kuachia shuti kali ambalo lilizama moja kwa moja langoni na kumuacha mlinda mlango wa Namungo FC Nurdin Barola akidaka upepo.
Mpaka wanakwenda mapumziko Simba walikuwa wanaongoza kwa idadi ya mabao 2-1 na mashabiki walikuwa hawana habari na mabao hayo bali furaha ya kubaki kileleni na kuwaacha watani zao nyuma kwa pointi 16.
Kipindi cha pili Namungo waliwasha moto na kusawazisha bao kupitia kwa Lusajo aliyeachia mshuti mkali nje ya 18 uliomshinda Kakolanya ila Kagere aliamsha furaha kwa kufunga dakika za lala salama akimalizia pasi ya Shiboub.
Simba imecheza jumla ya mechi 17 kwa sasa kwenye ligi na imejikusanyia jumla ya pointi 44 kibindoni ambazo ni nyingi kuliko za wapinzani wao Yanga wenye pointi 28 walizozipata kwenye mechi 15 walizocheza kwa sasa ndani ya ligi.
Yanga imebakiza mechi mbili mkononi ili kuwa sawa na Simba ila hata wakishinda mechi zote mbili zilizobaki bado mlima wa pointi utabaki kwao wataachwa kwa jumla ya pointi 10 ambazo wanapaswa wazitafute kwa udi na uvumba kuwapoteza wapinzani wao.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.