GUU la kulia na staili za mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, zimezua gumzo. Guu hilo limeweka rekodi kwa kuwaliza makipa sita wa Bongo tofauti na lile la kushoto lililomuotea kipa mmoja tu.
Lakini rekodi za msimu huu zinaonyesha bichwa lake pia ni balaa, limewalaza macho makipa watatu. Kwenye mabao yake 11, guu lake la kulia limekutana na makipa hawa; Farouk Shikalo wa Yanga (Simba 2-2 Yanga), Said Kipao wa Kagera Sugar (Kagera Sugar 0-3 Simba), Shaban Hassan wa Mtibwa Sugar(Simba 2-1 Mtibwa Sugar).
Richard Peter wa Mbeya City(Simba 4-0 Mbeya City) na Agathony Mkwanda wa Lipuli (Simba 4-0 Lipuli) waliokoteshwa mara mojamoja kila mmoja na Abdulrahman Mohamed wa JKT Tanzania aliokoteshwa nyavuni mara mbili wakati Simba ikishinda mabao 3-1. Kwa guu la kushoto ni Daniel Johannes wa Biashara United alikutana na balaa wakati Simba ikishinda mabao 2-0.
Ametupia jumla ya mabao matatu kwa kichwa ambapo aliwaokotesha nyavuni Mwadini Ally wa Azam FC,(Simba 1-0 Azam), Said Kipao wa Kagera Sugar(Kagera Sugar 0-3 Simba) na John Mwenda wa Alliance (Alliance 1-4 Simba), hawa wote aliwatungua bao mojamoja.
Post a Comment