BERNARD Morrison, nyota mpya wa Yanga amesema kuwa ataendelea kutoa burudani kwa mashabiki bila kuchoka kwani ni kitu anachokifikiria muda wote.
Morrison amecheza mechi mbili na amefunga bao moja akiwa na asisti mbili, mechi yake ya kwanza ilikuwa ni ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United na Yanga ilishinda mabao 3-1 alitoa asisti kwa Niyonzima na mchezo wa pili ulikuwa dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulikuwa ni wa Shirikisho na Yanga ilishinda mabao 2-0.
"Mambo bado yanakuja kwani huu ni mwanzo, ninachofikiri ni kuona namna gani nitawapa burudani mashabiki na kucheza mpira kwa umakini zaidi ya hapa kwani mambo bado yanakuja," amesema.
Post a Comment