IMEELEZWA kuwa kichapo cha mabao 2-1 walichopokea Mwadui FC kutoka kwa Simba kimepeperusha milioni mbili zilozokuwa mezani kwa ajili ya hamasa kwa wachezaji wa Mwadui FC.
Mwadui ilishindwa kufurukuta juzi, mbele ya Simba Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho na kupelekea kupoteza fuko hilo la mkwanja lilikuwa linawahusu.
Licha ya Gerald Mdamu kuanza kufunga bao dakika ya 34 halikudumu kwani Clatous Chama alisawazisha dakika ya 45+2 kabla ya Kahata kulipeperusha kabisa fuko la fedha kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 84.
Habari kutoka ndani ya Mwadui zimeeleza kuwa wachezaji wote waliahidiwa kupewa kila mmoja laki moja iwapo wangeshinda mbele ya Simba.
“Wachezaji wote waliahidiwa kupewa laki moja iwapo wangeshinda mbele ya Simba, mezani kulikuwa na dau la milioni mbili hivyo kupoteza kwao kumepeperusha fuko la hela zote zilizowekwa mezani na wadau,” kilieleza chanzo.
David Chakala, Meneja wa Mwadui FC amesema kuwa ni mpango ambao huwa unafanywa na Mwadui kutegemeana na mfuko wao ulivyo.
"Wakati mwingine huwa tunawaahidi wachezaji fedha za bonasi kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa wachezaji ila lengo ni kuona wanapambana na tunawasisitizia kwamba kazi ni yao kucheza, ila kuhusu hizo milioni siwezi kuzungumzia kwa sasa," amesema
Post a Comment