BAADA ya mshambuliaji wa JS Saoura, Thomas Ulimwengu kupata dili la kurejea kwenye Klabu yake ya zamani ya TP Mazembe ametuma ujumbe hwa wazi kwake namna hii:-
Thomas Ulimwengu umekuwa ukipambana sana lakini wengi wamekuwa wakikukatisha tamaa sana wakati hawajui safari yako ina mwendo na masahibu yapi.
Lawama, lawama, lawama na maneno ya chuki yanayoashiria ufahamu wenye lawama uliojaa chuki.
Kitu kizuri unaelewa na unajua unachohitaji, ndoto zako ni kwa ajili ya maisha yako. Wengi wanaolaumu hatujui wanataka nini na wamefanya nini katika ndoto zao na hujawahi kuwalaumu.
Endelea kusonga, TP Mazembe bado ni kubwa sana, kukusajili maana yake bado wanatambua uwezo wako.
Na Watanzania walipaswa kujivunia zaidi kuwa wewe mmoja wa wachezaji wa Kitanzania waliothubutu na kupata nafasi ya kucheza katika nchi za Afrika kama DRC, Sudan na Algeria ambazo zote ni bora kisoka kuliko Tanzania.
Mimi NAKUPA moyo, kurudi Mazembe si KUFELI badala yake ni mwendelezo wa safari ya maisha yako kisoka na Mungu ndiye anayejua mwisho wake... Umejitajidi sana, bila kupita Simba, Yanga wala Azam na leo ni mchezaji unayefahamika Afrika ukiwa na rekodi kibao.

Post a Comment