LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wawili ambao ni Ditram Nchimbi na Feisal Salum waliomba msamaha kwa kutimka kambini bila kuaga.
Habari zinaeleza kuwa, mshambuliaji, Nchimbi ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga akitokea Polisi Tanzania alilikokuwa kwa mkopo akitokea Azam FC na Fei Toto ambaye ni kiungo walikwea pipa kuelekea nchini Misri kufanya majaribio.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael alisema kuwa alikuwa akiskia taarifa kuhusu wachezaji wake hao wawili kuondoka ndani ya timu na hakuwa na taarifa kamili jambo ambalo sio sawa.
“Upo ndani ya timu na unakuwa unapata tu taarifa kutoka nje unadhani ni kitu kizuri? Sikutaka kuwafuatilia sana ila waliporudi kitu cha kwanza waliomba msamaha na nimewasamehe kwa sasa kazi inaendelea ,” amesema Eymael.
Yanga ipo nafasi ya nne kwenye ligi baada ya kucheza mechi 15, kibindoni imejikusanyia pointi zake 28, mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Mtibwa Sugar.
Post a Comment