ALIYEWAHI kuwa kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amemuangalia straika Muivory Coast, Yikpe Gnamien ambaye Yanga wanatamba naye, akasonya kwa sauti na kukunja sura kama mtu aliyekutana na pilipili kichaa bahati mbali kwenye pilau.

Yanga katika usajili wa dirisha dogo imesajili nyota sita wakiwemo wachezaji wa kigeni ambao ni Yikpe ili kuziba nafasi za wachezaji waliowaonyesha mlango wa kutokea.

Julio ambaye ni Simba kindakindaki, alisema kuwa, kiwango kilichoonyeshwa na Yikpe katika mechi alizocheza hakikumfurahisha hata kidogo na kudai kuwa ni bora nafasi hiyo akapewa mzawa.

“Yikpe unaona kabisa haendani na kiwango cha Yanga, ni vyema wanaokwenda kuchagua wachezaji maprofeshno lazima waangalie historia zao katika timu za taifa iwapo wanachezea ndipo waweze kuwapa nafasi ya kusajiliwa,” alisema Julio.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.