HUU hapa Ujumbe wa Mwandishi na mchambuzi wa masuala ya michezo Bongo, Saleh Jembe kwenda kwa Yanga:-

KWENU UONGOZI WA YANGA

Kamati ya mashindano kazi yake ni kuratibu ili timu ishiriki mashindano kwa uhakika. Lakini kinadharia na uhalisia, kamati haina uwezo wa kuhakikisha ushindi timu inapokuwa uwanjani otherwise kuna kitu kingine NJE YA MPIRA.

USHAURI..
Yanga iachane na matangazo ya namna hii yaliyopitwa na wakati, KUMBUKENI tupo 2020, mbali kidogo na zamani.

Uhakika wa ushindi ni wachezaji kujituma, kutumia maarifa na vipawa Mungu alivyowapa.

Kocha kufanya kazi yake kwa UFASAHA na kutengeneza mfumo bora na sahihi kuunganisha kikosi.


Yanga  kama wote ni wadau wa mpira, achaneni na madudu ya namna hii. Waiteni mashabiki waiunge mkono timu yao halafu IKISHINDA mfululizo, wala hamtasumbuka kuandika mambo kama haya.

Nawasilisha

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.