WAKATI nyota wa Yanga raia wa Ghana, Bernard Morrison, akiendelea kuwafanya wapenzi wa timu hiyo washindwe kuamini anachofanya uwanjani, kocha mkuu wa Yanga, Luc Eymael, anatarajia kushusha vifaa vingine zaidi yake.

Moja ya kifaa kingine kilichoshuka jijini kimyakimya ni raia mwingine wa Ghana, Joseph Quansah.

Quansa mwenye umri wa miaka 29 ametokea katika klabu ya Amodaus Professional na tayari ameshamwaga wino kuichezea Yanga miaka miwili.

Taarifa zinasema uwezo wake katika dimba la kati ni balaa kubwa huku naye akiwa na vionjo kama vya mtangulizi wake Morrison.

Morrison amekuwa gumzo jijini kutokana na vitu anavyofanya uwanjani, ambavyo mara nyingi wadau wa soka Tanzania walikuwa wakivishuhudia kupitia runinga wakati wanangalia mechi za nje.

Lakini safari hii, wanajionea wenyewe katika ardhi ya Bongo baada ya mchezaji huyo kusajiliwa kipindi cha dirisha dogo lililofungwa Januari hii na baadaye pacha wake naye anatua Jangwani.

Habari njema kwa Wanayanga wakati wakiendelea kupata burudani ya nyota hao, kocha wao Eymael ameahidi kukamilisha idadi yake kwa kushusha mchezaji mwingine ili kufikisha idadi ya watatu anaowahitaji kikosini.

Eymael ambaye ndiye aliyehusika kumleta nyota huyo, alisema anajua sehemu atakayowatoa wachezaji hao na alishindwa kuwasajili dirisha dogo baada ya kuchelewa kutua nchini.

“Morrison ni mchezaji mzuri, ila anahitaji wasaidizi katika kuimarisha safu yangu ya ushambualijia ili kufunga mabao mengi, nisingechelewa kuja ningesajili wachezaji wengine watatu kama huyu haraka.

“Hata hivyo bado lengo langu liko pale pale, nitatimiza wachezaji hao ili kuimarisha kikosi changu, nia yetu ni kutwaa ubingwa msimu huu ili kuleta furaha kwa Wana Yanga,” alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.