MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Yanga, David Molinga, amesema kuwa kazi ndiyo kwanza
imeanza Yanga, hivyo mashabiki wa timu hiyo wasiwe na hofu mambo mazuri
yanakuja.
Molinga ametoa kauli hiyo
baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United ambayo juzi
Jumatano ilichezwa kwenye Uwanja wa Namfua na kumalizika kwa Yanga
kushinda mabao 3-1, huku Molinga akiifungia moja kati ya hayo.
Akizungumza
na Championi Ijumaa, Molinga alisema kuwa mambo mazuri yanakuja Yanga
hivyo wapenzi na mashabiki wa timu hiyo hawatakiwi kukata tamaa. Alisema
hapo mwanzo kikosi kilikuwa bado hakijaelewana vizuri
lakini kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele wanazidi kuwa bora.
“Kwa
hiyo, kasi hii tuliyoanza nayo dhidi ya Singida ndiyo hiyo tutaendelea
nayo katika mechi zetu zote zilizobakia,” alisema Molinga ambaye sasa
ameshafunga mabao matano katika Ligi Kuu Bara wakati anayeongoza kwa
kuzifumania nyavu kwa sasa ni Meddie Kagere wa Simba, yeye ameshafunga
mabao 11.
SIMBA Kukusanya KIJIJI DODOMA / SENZO Ampa Neno MANARA “SEMEA Klabu Kote”

Post a Comment