KIKOSI
cha Simba, kesho Jumamosi kitashuka uwanjani kupambana na Mwadui FC
katika mchezo wa Kombe la FA utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam.
Hata hivyo, wapenzi na
mashabiki wa Simba wanaweza kumwona uwanjani Shiza Kichuya akiitumikia
timu hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kujiunga nayo hivi karibu akitokea
nchini Misri katika Klabu ya Pharco inayoshiriki Ligi Daraja la Pili
nchini Misri ambayo ilimsajili msimu uliopita akitokea Simba.
Katika
dirisha dogo la usajili lililofungwa hivi karibuni, Simba ilimsajili
Kichuya ambaye hapo awali alikuwa mmoja kati ya wachezaji wa kutumainiwa
wa timu hiyo kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji.
Habari
kutoka ndani ya Simba ambazo Champini Ijumaa limezipata zimedai kuwa,
kwa mara ya kwanza Kichuya anaweza kuonekana katika mchezo huo.
“Kichuya ameanza jana (juzi) mazoezi na timu baada ya kusajiliwa hivi karibuni, hata hivyo katika mazoezi hayo alionyesha uwezo mkubwa na kumvutia kocha.
“Kwa hiyo kama mambo yatakuwa vizuri basi katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Mwadui anaweza kuitumikia timu yetu kwa mara ya kwanza,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Hata
hivyo, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vanderbroeck alipoulizwa
alisema: “Ni mchezaji mzuri nimemuona mazoezini lakini siwezi kusema
kama nitamtumia au sitamtumia katika mechi hiyo.”
![]() |

Post a Comment