LEO Uwanja wa Uhuru utachezwa mchezo kati ya Simba na Tanzania Prisons zitakuwa kazini ikiwa ni mchezo wao wa kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo tangu Prisons ilipopanda daraja msimu wa 2011 ilipokuwa chini ya Kocha Mkuu Stephen Matata.

Mechi ya leo inatarajiwa kuwa ya ushindani kutokana na rekodi ambazo zimewekwa na wapinzani wa Simba, Prisons baada ya kucheza mechi 9 haijapoteza mchezo hata mmoja tofauti na wapinzani wao Simba ambao wamecheza mechi 8 na kupoteza mmoja mbele ya Mwadui FC.

Prisons inahaha kusaka rekodi mpya mbele ya Simba leo ambapo haijawahi kupata ushindi ikiwa ugenini tangu ilipopanda daraja msimu wa 2011, rekodi zo zipo hivi:-

Mechi zao kiujumla

Timu hizi zimekutana mara 14 huku Simba ikishinda mara 10, Tanzania Prisons imeshinda mechi mbili pekee na zote uwanja wa Sokoine huku zikitoa sare mbili.

Idadi ya mabao

Kwenye jumla ya mechi hizo 14 jumla ya mabao 25 yamefungwa huku Simba ikifunga jumla ya mabao 20 na Tanzania Prisons ikifunga mabao matano pekee.

Hattrick

Mechi moja ilileta mabao mengi zaidi ilichezwa uwanja wa Uhuru na Simba ilishinda kwa mabao 5-0 msimu wa  2014/15 uwanja wa Taifa na ilipatikana hattrick moja iliyofungwa na Ibrahim Ajibu.

Kadi nyekundu

Kwa upande wa kadi ni Simba pekee iliwahi kuonyeshwa kadi nyekundu kupitia kwa mchezaji wao Amir Maftah aliyemchezea rafu Khalid Fupi dakika ya 81 msimu wa 2012/13.

Nafasi zao kwa sasa

Simba inaongoza ligi ikiwa imecheza mechi 8 na imepoteza mechi moja mbele ya Mwadui FC ina jumla ya pointi 21 huku Tanzania Prisons ikiwa imecheza mechi 9 haijapoteza mchezo hata mmoja imeshinda mechi tatu na ina sare sita ikiwa na pointi 15 nafasi ya tano.

Matokeo yao yapo namna hii:
2012-13Simba 2-1 Prisons uwanja wa TaifaPrison 0-1 Simba uwanja wa Sokoine, 2013-14Simba 1-0 Prisons uwanja wa  TaifaPrisons 0-0 Simba uwanja wa Sokoine, 2014-15Prisons 1-1 Simba uwanja wa SokoineSimba 5-0 Prisons uwanja wa Taifa.

2015-16Prisons 1-0 Simba uwanja wa SokoineSimba 1-0 Prisons uwanja wa Taifa, 2016-17Prisons 2-1 Simba, uwanja wa SokoineSimba 3-0 Prisons uwanja wa Taifa, 2017-18Prisons 0-1 Simba uwanja wa SokoineSimba 2-0 Prisons uwanja wa Taifa, 2018-19Simba 1-0 Prisons uwanja wa TaifaPrisons 0-1 Simba uwanja wa Sokoine.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.