Home
Unlabelled
Samatta baada ya kupokea comments zinazodai hachezi vizuri Taifa Stars
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ametumia ukurasa wake wa twitter kueleza msimamo wake, baada ya kupokea comments mbalimbali za mashabiki wa soka Tanzania wakimtuhumu kuwa hajacheza vizuri Taifa Stars katika mchezo dhidi ya Libya, Tanzania ikipoteza 2-1.
“Nimepata meseji na comment kutoka kwa watu kadhaa kuwa awajaelewa kiwango nilichoonesha ktk mechi za timu ya taifa, anyway ukweli nimefurahi kuona watu wanasema ukweli sichukulii binafsi bali nachukulia km chachu itakayonifanya nijitume zaidi ili niweze Bora zaidi, HAINA KUFELI”>>> Samatta
Tunisia wao wameendeleza kuongoza katika msimamo wa Kundi J wakiwa na point 6, Libya point 3(head to head) dhidi ya Tanzania inambeba na Tanzania nafasi ya 3 wakiwa na point 3 na Equatorial Guinea wakiwa wa mwisho kwa kwa kuwa na point 0.
Post a Comment