LICHA ya kusuasua katika kuzifumania nyavu katika michezo ya hivi karibuni ya Ligi Kuu Bara, mshambuliaji wa Yanga Mkongomani, David Molinga amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo akiwahakikishia kufunga mabao kwenye mechi zijazo.



Wikiendi hii katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union, Molinga alikosa penalti jambo lililowakera mashabiki wakati huo timu yao ikiwa nyuma bao 1-0.



Mkongomani huyo hadi hivi sasa tayari amefunga mabao mawili akicheza michezo mitano ya ligi tangu ajiunge na timu hiyo akitokea nyumbani kwao, DR Congo.



“Ndiyo uhalisia wa mpira, kuna kufanya vizuri muda mwingine vibaya, juzi sikuweza kufunga lakini nimepambana kuchangia ushindi wa mabao 3-1 tulioupata tulipokutana na Coastal.



“Ninaamini mchezo ujao nitarejea kwa kishindo na kuweza kufunga ama kuisaidia kushinda timu yangu, imekuwa siku mbaya kwangu kwa kutokufunga tulipocheza na Coastal,” alisema Molinga.



Yanga imepanga kuongeza washambuliaji wawili kwenye usajili wa dirisha msimu huu katika kukiboresha kikosi chao kati ya wachezaji wanaotajwa kuachwa ni Maybin Kalengo, Issa Bigirimana, Sadney Urikhob na Juma Balinya

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.