KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Patrick Sibomana amesema kuwa ilikuwa lazima wapate ushindi dhidi ya JKT Tanzania ili kuzidisha imani kwa mashabiki wa klabu hiyo. 

Yanga walipata ushindi wao wa nne msimu huu baada ya kuwafunga JKT Tanzania kwa mabao 3-2 kwenye mchezo uliopigwa juzi, Ijumaa kwenye uwanja wa Uhuru, Jijini Dar.

 Mabao ya Yanga yalifungwa na Patrick Sibomana dakika ya 
12, Juma Balinya dakika ya 23 na David Molinga aliyefunga kwa faulo dakika ya 35, huku ya JKT yakifungwa na Adam Adam dakika ya 13 na Danny Lyanga dakika ya 45.

 Akizungumza na Spoti Xtra Sibomana alisema;
 “Tangu tulivyoingia uwanjani kila mchezaji alikuwa anajua lazima tushinde ili kujenga imani kwa mashabiki, tunataka kuwaaminisha mashabiki wetu kuwa timu yao ni nzuri na wawe na imani nayo.” 

Yanga sasa wamecheza michezo sita na kuvuna alama 13, wakishinda michezo sita, kupoteza mmoja na kutoka sare mmoja

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.