NAFASI ya mshambuliaji mpya wa Simba, Wilker da Silva ndani ya kikosi cha kwanza inazidi kuwa finyu huku taa nyekundu zikiwaka kichwani mwake licha ya kufunga hivi karibuni bao mbele ya JKT Tanzania mchezo wa kirafiki na Simba ilishinda bao 1-0 mabosi wameguna.
Silva ambaye alijiunga na Simba msimu huu akitokea Brazil ameshindwa kufurukuta kwenye ligi ya Bongo alicheza dakika tatu tu mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar jambo linalofanya mabosi kumjadili upya.
Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa miongoni mwa wachezaji watakaopigwa chini mazima ni pamoja na Wilker.
"Ndani ya Simba kuna wachezaji kama tisa hivi wanatakiwa kuachwa miongoni mwao ni huyu Wilker kwani hajaonyesha makali yake na wapo wengine ambao wanaweza kutolewa kwa mkopo.
"Suala la kufunga haimaanishi ndo unajua mpira tunaangalia mchango wake ndani ya timu, kuna usukaji wakikosi unakuja," kilieleza chanzo hicho.
Mtendaji Mkuu wa Simba hivi karibuni alisema suala la kuwaacha wachezaji ndani ya Simba ambao hawajaonyesha uwezo haliepukiki na orodha yao ipo tayari.
"Kuwaacha wachezaji ni suala linalotokea kwenye timu zote hivyo kwa sasa kunahitaji utulivu na umakini mkubwa ili kuwapata walio sahihi," amesema Mazingisa
Post a Comment