Wachezaji wa Ajax na Heracles hawakucheza mpira katika dakika ya kwanza ya mchezo wao wa ligi jana ikiwa ni ishara ya kupinga ubaguzi wa rangi.
Klabu za madaraja mawili ya juu nchini Uholanzi zilikubaliana kufanya hivyo wikiendi hii baada ya winga Ahmad Mendes Moreira wa klabu ya Excelsior kufanyiwa ubaguzi wa rangi na mashabiki Den Bosch katika mechi ya ligi daraja la pili wiki iliyopita.
Post a Comment