Baada ya kurejeshwa kundini ndani ya klabu ya Yanga katika nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Mashindano, Salum Mkemi, amesema amefurahia kurejeshwa ndani ya mabingwa wa kihistoria.

Mkemi amerejea ikiwa ni miezi kadhaa tangu aachie wadhifa huo kutokana na mambo kadhaa kutokuwa sawa ndani ya klabu hiyo.

Kiongozi huyo ambaye ni shabiki damu na mwanachama wa Yanga, amesema ni faraja kubwa kwake kwani kitendo cha kurejeshwa wakati alikuwa ameachia ngazi kinaonesha alikuwa na msaada ndani ya timu.

"Kwakweli nimefarijika sababu kitendo cha kuitwa wakati nilikuwa nimeondoka Yanga kina maana kubwa.

"Mimi naipenda Yanga, ni shabiki na mwanachama, nimefurahi kuona jina langu likitangazwa tena

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.