Baada kuziona nyavu kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki wa timu yake ya Simba, Mbrazil Wilker Da Silva amesema sasa ni muda wa kupambana bila kujali aina ya mpinzani wanayekwenda kukutana naye.
Da Silva aliifungia Simba bao pekee wakati ikishinda 1-0 kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya JKT
Tanzania iliyopigwa Uwanja wa Chamazi Ijumaa, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa mshambuliaji
huyo kufunga bao akiwa na Simba katika ardhi ya Tanzania, kwani mabao mengine aliifungia wakati
ikiwa kambini Afrika Kusini kabla ya msimu kuanza.
Kufuatia furaha hivyo, Mbazil huyo amesema: "Nilifurahi sana baada ya kufunga bao. Simba ni timu
kubwa na tunapaswa kupambana ili kushinda kila mchezo bila kujali aina ya mpinzani ambaye
tunakutana naye."
Simba inayoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, itashuka katika Uwanja wa Uhuru kesho
kuikaribisha Ruvu Shooting ambayo itakuwa ikihitaji ushindi ili kuendeleza ubabe wake dhidi ya
vigogo wa soka nchini baada ya awali kuichapa Yanga.
Katika mechi hiyo, Simba inatarajiwa kuongozwa na Kocha Msaidizi, Dennis Kitambi, kufuatia Kocha Mkuu, Mbelgiji Patrick Aussems kuzuiwa kwa muda na uongozi wa klabu hiyo kutokana na kukerwa na tabia yake ya kuondoka nchini na kudai kwenda kwao Ubelgiji kwa matatizo binafsi bila ruhusa
Post a Comment