Mkasa aliokutana nao Haji Manara akiwa Tunisia alipoenda kuipa sapoti Taifa Stars katika mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON dhidi ya Libya.
Anaandika...
Nimekuwa wa mwisho kurejea nyumbani kama nilivyokuwa wa mwisho kufika hapa Tunisia.
Nilipata changamoto kubwa sana hapa ya kupoteza passport, kiukweli ilikuwa ni bahati tu kuja kuipata na ndiyo maana nimeachwa peke yangu katika nchi hii isiyozungumza kabisa kingereza!!
Nawashukuru wote waliofanikisha kupatikana kwa passport yangu. Na niwashukuru maafisa ubalozi wetu wa France ambao pia wanatuwakilisha Tunisia kwa jitihada zao.
Narejea kwa Safari ndefu ya kutoka hapa kupitia Istanbul hadi Lusaka kisha kwa Bi Mkubwa!!
Hakika Watanzania ni watu wema na wakarimu hasa tunapokuwa ugenini... Alhamdulillah 🙏
Post a Comment