Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolous Musonye, amesema kuwa tangu achukue kiti hicho hajawahi kufanya kitu kibaya akiwa madarakani.
Musonye amefunguka hayo ikitajwa hivi karibuni CECAFA watakuwa na uchaguzi kwa ajili ya kuchagua viongozi wapya.
Akizungumza kupitia Clouds FM, licha ya kutoa taarifa za uchaguzi, Musonye amesema amekuwa akigombana na timu za Simba na Yanga kwa sababu ya kuwapa changamoto.
Kiongozi huyo wa muda mrefu ameeleza kukiri kuwa ni kweli Simba na Yanga zimekuwa na msisimko mkubwa pale zinaposhiriki katika mashindano yanayoandaliwa na CECAFA.
"Ujue Simba na Yanga kiuhalisi zimekuwa na msisimko mkubwa zinaposhiriki mashindano ya CECAFA.
"Tumekuwa tunagombana mara kadhaa pale inapotokea wamekataa kushiriki lakini hizo ni siasa za mpira tu na wala hawana tatizo kabisa.
"Nakubali mchango wao mkubwa ndani ya CECAFA, hutokea hasira za hapa na pale lakini huwa hazikai muda mrefu
Post a Comment