Wakati akitarajia kuanza kucheza katika kikosi cha kwanza muda wowote kutoka sasa, straika na nahodha wa Simba, John Bocco, ameweka wazi kwamba pacha yake na Meddie Kagere itafunga mabao mengi.
Bocco amesema hayo licha ya kwamba hadi sasa bado hajacheza hata mechi na Kagere kutokana na kuwa majeruhi.
Bocco na Kagere kwa sasa ndiyo wanatazamiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba katika michezo ya ligi ikiwa baada ya kucheza sambamba tangu msimu uliopita.
Straika huyo ameliambia Championi Jumatatu, kuwa licha ya kwamba wameshindwa kucheza sambamba yeye na Kagere hadi sasa lakini anaamini atakaporudi na kuunganisha pacha hiyo watazisumbua timu nyingi za ligi kuu.
“Kitu kibaya ni kwamba hadi sasa mimi na Kagere hatujacheza sambamba pamoja tukiwa wawili. Tulicheza msimu uliopita lakini tulikuwa watatu mimi, Kagere na Okwi kwa hiyo ikatunyima nafasi ya kucheza sambamba.
“Niseme tu wazi kuwa naona kabisa tutasumbua wakati ambao tutacheza pamoja nikitoka katika majeruhi ambayo yamechangia kwa kiwango kikubwa kutocheza hadi sasa katika timu,” alisema Bocco
Post a Comment