Nyota wa timu ya Simba, Miraj Athuman, ‘Sheva’ amesema kuwa mshambuliaji mwenzake wa Simba, Meddie Kagere ni habari nyingine kwa wafumania nyavu bongo kutokana na uchu wa kufumania nyavu alionao.

Sheva ameifungia Simba jumla ya mabao manne na ametoa asisti moja kwa sasa yupo na timu ya taifa ambayo jana ilikuwa inamenyana na Libya nchini Tunisia mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon 2021  nchini Cameroon.

Sheva alisema kuwa uwepo wa Kagere ndani ya Simba unamfanya achangamke na kupambana kufikia rekodi yake kutokana na jitihada za Kagere akiwa ndani ya uwanja.

“Kagere ni mshambuliaji wa aina yake, akiwa ndani ya uwanja hatulii mpaka apate kile anachokitaka jambo ambalo limekuwa likiniongezea morali nami nikiwa uwanjani bila kujali nipo na timu yangu ya Simba ama na timu ya taifa.

“Vitu vingi najifunza kutoka kwake ukizingatia yeye ana uzoefu kuliko mimi ni wakati wangu kufanya mazuri kwa ajili ya mashabiki na taifa kiujumla kwani bado nina muda wa kufanya mengi zaidi,” alisema Sheva.

Kagere ni mfungaji bora kwa msimu uliopita ambapo alifunga jumla ya mabao 23 na sasa ana mabao nane akiwa ndiye kinara wa ufungaji kwenye ligi

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.