Straika hatari wa Polisi Tanzania na Taifa Stars, Ditram Nchimbi, amesema kuwa hajazungumza na Yanga juu ya kutaka kumsajili.
Nchimbi amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa jitihada zake zote na majukumu ya mpira bado yatasalia kwa Polisi Tanzania.
Ameeleza mazungumzo mengine yatakuja mara baada ya kumaliza mkataba na Azam na kwa sasa hawezi kuzungumza mengi kwa kina.
Imekuwa ikielezwa kuwa mabosi wa Yanga wamekuwa wakipambana kufa na kupona ili kupata saini ya mchezaji huyo ambaye ni tegemo katika kikosi cha Polisi ambacho anakichezea kwa mkopo
Post a Comment