JOSE Mourinho amerejea kwenye kazi ya kuwa kocha mkuu baada ya kupita siku 338 alipotimuliwa kukinoa kikosi cha Manchester United kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho ndani ya Ligi Kuu England. Hivi sasa amepewa kazi na mabosi wa Tottenham Hotspur.

Mchezo wa kwanza wa Mourinho ambaye aliwahi kuinoa pia Chelsea utakuwa dhidi ya Westham United utakaochezwa Jumamosi ya wikiendi hii.
         
         Mourinho amepewa mkataba unaomalizika msimu wa 2022/23 akipokea mikoba ya Mauricio Pochettino ambaye alidumu ndani ya Spurs kwa muda wa miaka mitano akiwa ni kocha mkuu.

Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy amesema kuwa hawakuwa na chaguo lingine la kufanya kwa Pochettino kutokana na maamuzi ambayo walikubaliana na bodi jambo lililoafikiwa na kila mmoja kuachana naye.
Sababu kubwa ambazo zinaelezwa zimechangia kocha huyo kupigwa chini ni mwelekeo wa kusuasua wa timu hiyo kwenye Ligi Kuu England ambapo ipo nafasi ya 14 pia kichapo cha mabao 7-2 wakiwa nyumbani kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Oktoba, mwaka huu, kilibadili upepo wa kocha huyo

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.