HARRY Kane mshambuliaji wa Tottenham Hotspur leo amefikisha jumla ya mabao 7 kwenye premier League baada ya kufunga bao la tatu kwenye ushindi wa mabao 3-2 mbele ya West Ham.
Mchezo wa leo ambao ulikuwa wa kwanza kwa Jose Mourinho kukaa kwenye benchi akipokea mikoba ya Mauricio Pochentino ulikuwa na ushindani wa kipekee kwa timu zote.
Son Heung-min alianza kupachika bao la kwanza dakika ya 36 na Lucas Moura alipachika bao la pili dakika ya 43 na la ushindi likipachikwa na Kane dakika ya 49.
West Ham ilizinduka dakika ya 73 na kupachika bao lao la kwanza kupitia kwa Michail Antonio kabla ya lile la pili kupachikwa dakika ya 90+6 na Angelo Ogbonna.
Ushindi huo unaifanya Tottenham Hotspur kuwa nafasi ya 9 ikishinda mchezo wake wa nne na inafikisha jumla ya pointi 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England
Post a Comment