STAA wa Real Madrid, Eden Hazard, amemsifia mshambuliaji wa timu hiyo, Karim Benzema kwa kusema hivi sasa ndiye mshambuliaji bora na hakuna wa kupinga hilo.

Wachezaji hao wawili wamekuwa wakicheza pamoja katika klabu hiyo msimu huu, huku Benzema akicheza namba tisa na Hazard kumi.

Hazard ambaye amejiunga na klabu hiyo msimu huu akitokea Chelsea, alisema kuwa staa huyo ni mshambuliaji bora kwa sasa kutokana na uwezo wake.

“Baada ya kucheza na Benzema kama mieizi mitatu, kwangu mimi naona ndiye straika bora kwa sasa duniani kutokana na uwezo wake.

“Ukiachana na kuwa bora, lakini bado anatufanya hata sisi wachezaji wengine kuwa bora uwanjani kwa jinsi ambavyo tunacheza naye.

“Ni rahisi kucheza na timu ambayo inakuwa haina Benzema ndani, hii namaanisha pale tunapocheza timu mbili tofauti ndani ya Real Madrid,” alisema Hazard na kuongeza.

“Tangu niwe hapa mambo yanakwenda vizuri, tunashinda na timu imekuwa ikiimarika jambo ambalo linafanya mambo kuwa mepesi kwa upande wangu.”

Benzema msimu huu amefunga mabao 11 katika michuano ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Hazard akiwa na bao moja tu katika mechi saba za La Liga

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.