HASSAN Mwakinyo bondia wa ngumi za kulipwa Bongo amesema kuwa hajafurahishwa na aina ya ushindi alioupata mbele ya Arnel Tinampaya.
Kwenye pambano la rauundi 10 lililopigwa uwanja wa Uhuru, Mwakinyo alishinda kwa pointi jambo ambalo hajafurahia.
"Sijafurahia aina ya ushindi niliuupata ila ni sehemu ya matokeo kwa kuwa ushindani ulikuwa mkubwa na gloves hazikuwa rafiki kwangu, wakati mwingine nitakuwa tofauti zaidi ya hapa," amesema Mwakinyo.
Matokeo ya jumla yapo namna hii:-Jaji wa kwanza ametoa 97 -93 , Jaji wa pili akatoa 98-92 na Jaji wa tatu akatoa 96-96.
Post a Comment