FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa wachezaji wake wanatakiwa kupambana kila wanapocheza na timu zilizo nafasi ya juu kwenye msimamo.

Chelsea ilichapwa mabao 2-1 na Manchester City mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa Uwanja wa Etihad.


 "Kama tunahitaji kutwaa ubingwa au kufanya vizuri kwenye ligi lazima tukubali kupambana na Liverpool, Spurs, Manchester City na timu nyingine zote kubwa. 

"Wachezaji wangu wanapaswa kupambana sana kila wanapocheza na hizi timu sita za juu," amesema.

Chelsea ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi zake 26 nyuma ya pointi 11 ya Liverpool waliopo kileleni

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.