Mshambuliaji wa Polisi Tanzania na Taifa Stars, Ditram Nchimbi, ameibuka na kusema hajafanya mazungumzo yoyote na klabu ya Yanga juu ya kumsajili.

Nchimbi ambaye akuwa kwenye kwenye kiwango kizuri hivi karibuni mpaka kuepelekea kuitwa Stars na Kocha Etienee Ndayiragije, amekanusha taarifa zilizosambaa kuwa tayari kaongea na mabingwa hao wa kihistoria kunako Ligi Kuu Bara.

Kufutia kukanusha taarifa hizo, Nchimbi amewataka Yanga kama kweli wamedhamiria kumsajili wazungumze na uongozi wa Polisi na wakishafikia mwafaka atakuwa tayari kuungana nao.

Hivi karibuni imekuwa ikielezwa Yanga wamekuwa wakiwania saini ya mchezaji huyo ambaye aliwafunga mabao matatu pekee katika mechi waliyokutana kwenye ligi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.