Wakati mashabiki wengi wa Simba wakiwa na presha ya kutwaa ubingwa kutokana na kutopata matokeo mazuri katika mechi zao mbili za mwisho za Ligi Kuu Bara, nahodha na straika wa kikosi hicho, John Bocco amewatuliza presha kisha akawapa ahadi ya kutia nguvu.
Bocco amewatuliza mashabiki wa timu hiyo presha walizonazo kwa kuwaambia hata iweje watapambana kwa nguvu zote kuona wanachukua tena ubingwa wa ligi kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki hao lakini kujihakikishia nafasi ya kucheza kimataifa mwakani.
Straika huyo ambaye hajacheza mechi yoyote ya ligi hadi sasa akiwa majeruhi, ameliambia Championi Jumatatu, kuwa ana uhakika mkubwa wa wao kutwaa kwa mara nyingine tena ubingwa wa ligi kutokana na aina ya mwenendo ambao wamekuwa nao katika ligi hadi sasa.
“Hadi muda huu hatujawa na mwenendo mbaya kabisa katika ligi kwa sababu tumeshinda mechi saba, tumepoteza moja na kutoa sare moja.
“Bado tuna nafasi kubwa sana kwa sababu zimebaki mechi nyingi ambazo tuna uwezo kabisa wa kufanya vizuri, niwaambie kwamba tutawapa furaha kwa kuchukua ubingwa mwa mara nyingine tena. Tuna huo uwezo na tutalikamilisha suala hilo niwaambie,” alisema Bocco
Post a Comment