Wachezaji wa ngazi ya juu wa Arsenal wanahofia kuwa wachezaji wao maarufu watalazimika kuangalia upya mustakabali wao wa baadae ikiwa meneja Unai Emery ataendela kushikilia wadhifa huo msimu ujao .(Mail)
Mshambuliaji wa England Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 24, anasubiri kuona ikiwa meneja wa Manchester City Pep Guardiola atajitolea kuiboresha klabu hiyo kabla ya kusaini mkataba mpya . (FourFourTwo)
Guardiola amezionya klabu zenye haja na naibu wake kwamba Mikel Arteta, ambaye ametokea kuwa mgombea anayeongoza katika kuchukua ya ukufunzi wa Arsenal na Everton, ataendelea kubakia katika City kwa walau kipindi kilichobaki cha msimu. (Times)
Meneja wa Tottenham Jose Mourinho amemuomba wakala Jorge Mendes kuendelea kumpa taarifa kuhusu wachezaji Ruben Dias mlinzi katika klabu ya Benfica ya Ureno mwenye umri wa miaka , 22, pamoja na kiungo wa kati Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 25, wa klabu ya Sporting Lisbon. (90min)
West Ham wanaangalia uwezekano wa kumchukua meneja wa Sheffield United Chris Wilder kama meneja wao ajaye, ikiwa wataamua kumfuta kazi meneja wao sasa Manuel Pellegrini. (Mirror)
Pellegrini tayari ameonywa kwamba matokeo ya timu lazima yawe bora wakati wa mazungumzo na bodi ya the Hammers. (Times)
Meneja wa Everton Marco Silva anaweza kupewa fursa ya kuongoza gemu mbili zaidi iwapo mhisani wakuu Farhad Moshiri na mwenyekiti wa klabu hiyo Bill Kenwright watakuwa wakijadili juu ya meneja mbadala. (Mail)
Kocha wa zamani wa Toffees Sam Allardyce anasema ni wazi wachezaji hawachezi tena kwa ajili ya Silva. (Talksport)
Mkurugenzi wa soka wa klabu ya Everton Marcel Brands na meneja Silva wamefanya mazungumzo juu ya mkakati wa kumrejesha katika klabu hiyo mlinda mlango mreno Joao Virginia kutoka Reading anakocheza kwa mkopo(echo)
The Foxes walilazimika kumzuia mlinzi kutoka Croasia mwenye umri wa miaka 22 Filip Benkovic kwenda Stoke City kwa mkopo katika msimu uliopita baada ya kushindwa kusaini mkataba na Harry Maguire ambaye alitarajiwa kuziba pengo lake. (Athletic, via Leicester Mercury)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema "anampenda" mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 20, huku klabu yakeikijiandaa kuwapokea Paris Saint-Germain katika Ligi ya mabingwa. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Chelsea mfaransa N'Golo Kante anasema uamuzi wake wa kutohamia katika klabu ya Ufaransa PSG ulikuwa ni "wa kimchezo" (Canal Plus, via Mirror)
Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis ameitoza faini ya zaidi ya pauni milioni 2.1 kwa timu ya kwanza kufuatia "uasi ndani ya klabu ". (ESPN)
Mlinzi wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, mwenye umri wa miaka 26, amesema haiwezekani kurudi Lyon huku, klabu ya Arsenal ikimtaka. (Sport)
Wakala wa mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling wamesafiri hadi Italia kuanza mazungumzo juu ya uhamisho wa kudumu na Roma, baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kuivutia timu hiyo kuanzia mwanzo wa msimu huu. (Corriere della Sera via Mail)
Kiungo wa kati wa England na Tottenham Dele Alli, mwenye umri wa miaka 23 alihisi mwenye majuto kufuatia kufukuzwa kazi kwa meneja wa zamani Mauricio Pochettino. (Mail)
Post a Comment