Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amemtaka Kocha Mkuu wa taifa Stars, Mrundi, Etienne Ndayiragije, kutoona aibu ya kumuanzisha benchi mshambuliaji Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji.

Kauli ya Julio imekuja kufuatia Samatta kushindwa kung'ara juzi katiia mechi ya kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Libya ambayo Stars ilipoteza kwa mabao 2-1.

Julio amesema Ndayiragije asiwe na hofu ya kumuanzisha benchi Samatta ili apate fursa na nafasi ya kuusoma vizuri mchezo ili aweze kufanya vema na aendane na timu vizuri.

"Inabidi Ndayiragije asione aibu kumuanzisha Samatta benchi ili ausome vizuri mchezo.

"Unaona kama mechi ya juzi alicheza lakini mechi ilikuwa imemkataa kabisa, ili kuepusha haya yanayotokea vema akawa hamwanzishi," amesema Julio

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.