Mchezaji Samuel Eto'o Staa wa zamani wa vilabu vya Barcelona, Inter Milan na Chelsea, baada ya kutangaza kustaafu kucheza soka mwezi Septemba ameeleza ni kwanini ana mipango ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Harvad.

Eto'o ataanza masomo yake ya usimamizi wa biashara katika Shule ya Biashara ya Harvad (Havard Business School) Januari 2020.

"Nataka kusaidia na kutoa mchango wangu mzuri kwa mabadiliko ya bara letu, unapokuwa mchezaji wa mpira wa miguu, hunalipa watu ili wasimamie kazi yako na mambo yako kwa ujumla," alieleza.

Aliendelea kwa kusema, "Lakini wakati unapofika ni zamu yako unataka kusimamia watu wengine na unataka kuwaendeleza, unahitaji kujifunza ujuzi mpya".

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.