Timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imepangwa Kundi C katika michuano ya Mataifa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Senior Challenge Cup 2019) ikiwa pamoja na wanafainali wa michuano iliyopita, Kenya na Zanzibar.

Michuano hiyo imepangwa kuanzia Desemba 7 hadi 19 mwaka huu nchini Uganda na itakufikia mubashara kupitia Azam Sports 2 ikishirikisha timu 12 ikiwemo DR Congo kama timu mwalikwa.

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amesema DR Congo wamekubali kushiriki michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi kuelekea Fainali ya Mataifa Bingwa Afrika (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon.

Katika droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, timu hizo 12 zimepangwa katika makundi matatu kama ifuatavyo.

GROUP A
1. Uganda
2. Burundi
3. Ethiopia
4. Eritrea .

GROUP B
1. DRC Congo
2. Sudan
3. S. Sudan
4. Somalia .

GROUP C
1. Kenya
2. Tanzania
3. Djibouti
4.Zanzibar

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.