Imeripotiwa kuwa Kocha wa Simba, Patrick Aussems tangu mechi ya Ruvu Shooting amesimamishwa kufanya kazi yoyote ndani ya klabu hiyo.

Taarifa imesema maamuzi hayo yamekuja kufuatia makosa mbalimbali aliyoyafanya Aussems ndani ya timu ikiwemo la kuondoka nchini bila ruhusa ya mabosi wake.

Mbali na kuondoka bila ruhusa, inaelezwa pia Aussems aligoma kukaa kitako na Ofisa Mtendaji wa klabu, Senzo Mazingisa ambacho kililenga kujadili mambo kadhaa kuhusu timu siku chache zilizopita.

Ukaichana na sababu tajwa hapo juu, inaelezwa pia kuwa uwezekano wa Aussems kuondoshwa ndani ya Simba upo kutokana na mwenendo wa kikosi cha timu ulivyo.

Inavyosemekana ni kuwa Aussems amekuwa na urafiki uliopitiliza na wachezaji kiasi cha kwanza inapelekea baadhi ya wachezaji kuwa na changamoto ya nidhamu jambo ambalo limechukuliwa kitofauti

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.