Baada ya kuondolewa kwa kocha mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera na nafasi yake kukaimiwa na Boniface Mkwasa, mchezaji wa zamani na kocha wa magolikipa wa Yanga SC Juma Pondamali ameeleza sababu zake za kuamua kuondoka Yanga SC kabla ya kuanza kwa msimu wa 2019/20.
Pondamali akihojiwa na Clouds FM alieleza kuwa aliamua kuomba kuondoka Yanga kwa sababu tu aliona club hiyo imekusanya na kuchangiwa michango na nchi nzima, kitu ambacho anadai hajawahi kukiona katika club yoyote, hivyo anaamini presha ingekuwa kubwa kama ilivyo sasa kwani mashabiki wangedai matokeo kila mechi.
Post a Comment