Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Etienne Ndayiragije amesema moja ya sababu ya kuacha kwa Mlinda mlango wa soka wa Simba Aish Manula ni kuwa mchezaji huyo kucheza michezo katika timu yake ya Simba na timu ya Taifa kwa msimu uliopita na kupelekea kushindwa kufanya vizuri
kwenye timu ya Taifa.

Kocha Ndayiragije ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kipenga cha East Africa Radio kinachoruka kila siku kuanzia saa 2 usiku, ambapo amesema kuwa kwa msimu uliopita Simba ilifika mbali sana Kimataifa kwenye Klabu Bingwa Afrika, lakini pia timu ya Taifa ilienda mpaka michuanio ya AFCON.

"Mechi alizocheza Aishi Manula mwaka jana zilimzidi kwa sababu @SimbaSCTanzania ilifika mbali Kimataifa, pia timu ya Taifa ilienda mpaka AFCON, kwa hiyo tuliangalia utaratibu wa kumpumzisha, kwa hiyo hawezi kushuka kiwango' amesema Kocha Ndayiragije

Aidha Ndayiragije amesema kuwa "kuhusu Manula na Kaseja kwenye uwezo wao kuitwa timu ya Taifa, mara nyingi huwa tunaita wachezaji kulingana kiwango chake kwa wakati huo, lakini pia tunaangalia kama atakuwa na kiwango hichohicho tulichokiona ndani ya Klabu"

Aidha Kocha huyo amesema ameomba muda wa kutosha kwa ajili ya kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Kimataifa ikiwemo ya CHAN

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.