Kiungo wa Borussia Monchengladbach, Denis Zakaria, Mathieu Bed, amesema staa huyo kwa sasa hawezi kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Zakari amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu za Manchester United, Liverpool na Arsenal ambazo zote zikiwa ni za Ligi Kuu ya England.

Wakala huyo alisema kwa sasa hawana mpango wa kumtoa mchezaji huyo kipindi hiki cha kuelekea usajili wa Januari, mwakani.

Tayari kigogo wa Man United, Ed Woodward alitamka wazi kuwa ana mpango wa kumvuta nyota huyo ambaye ataziba pengo la Ander Herrera aliyetimkia PSG mwanzoni mwa msimu huu.

Wakala huyo alifunguka kuwa: “Denis hataondoka Borussia kipindi hiki cha majira ya baridi, kwa sasa yupo vizuri, amekuwa akifanya vizuri anahitaji kubaki hapa Gladbach sababu bado kuna vitu anataka kuonyesha akiwa hapa.”

Beda aliendelea kusisitiza kuwa, klabu ambazo zinamuhitaji mchezaji huyo zinatakiwa kusubiri kipindi cha majira ya joto ndipo wanaweza kumnunua.

Zakaria alijiunga na klabu hiyo 2017 akitokea Young Boys, kwa sasa amekuwa akifanya vizuri ndani ya Bundesliga

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.