OBREY Chirwa mshambuliaji wa Azam FC leo amekuwa shujaa mbele ya Alliance FC wakati Azam FC ikishinda mabao 5-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Nyamagana leo Novemba 26.

Chirwa alianza kuandika bao la kwanza dakika ya nne huku lile la pili akapachika dakika ya 25 kabla ya Idd Chilunda kupachika bao la tatu dakika ya 33 na kuifanya Azam FC kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili Alliance walitulia na kusoma hesabu za Azam FC kosa moja liliwagharimu dakika ya 53 kwa kumruhusu Chilunda kuandika bao la nne kwa Azam na la pili kwake kabla ya msumari wa tano kupachikwa na Chirwa dakika ya 68. 

Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa Azam FC ikiwa kanda ya ziwa kwani walianza kuitungua Mbao FC bao 1-0 na leo wameitungua mabao 5-0 Alliance FC

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.