Wachezaji watatu wa Klabu ya Yanga, Lamine Moro, Ally Ally na Mohamed Banka waliokuwa majeruhi wamepona na wamerejea kikosini.
Wachezaji hao wamerejea tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa leo November 22 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kurejea kwa wachezaji hao kunatoa mwanga kwa Yanga kufanya vizuri katika mechi hiyo kutokana na kuimarisha kikosi chake.
Yanga inaenda kukutana na JKT Tanzania ikiwa i mech yake ya pili tangu Boniface Mkwasa atangazwe kuwa Kaimu Kocha kufuatia Mwinyi Zahera kufukuzwa kazi
Post a Comment