Aliyekuwa kocha wa Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike raia wa Nigeria ameomba kazi ya kufundisha timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo'.

Ikumbukwe Amunike alifukuzwa kazi Tanzania baada ya kuwa na mwenendo mbaya ndani ya kikosi cha Stars.

Hivi karibuni Amunike alihojiwa na kituo cha habari cha BBC na kusema kuwa anatafuta kazi sababu mpaka sasa hana kibarua chochote.

Maombi yake ya kazi kwenda Chipolopolo yameungana na makocha wengine ambao wameomba kazi ndani ya timu hiyo ambayo ni kongwe ndani ya ukanda wa Afrika katika mashindano ya kimataifa.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.